MBINU ZA MAFANIKIO KWENYE BIASHARA YAKO

MBINU ZA MAFANIKIO KWENYE BIASHARA


1.Fanya kitu unachokipendaa:

 Hapa unalazimika kuekeza  Hela zako, Muda wako , Ujuzi wako ili kujipatia Matokeo Makubwa ya Mafanikio Katika Maisha yako.


Usikubali kwenye Maisha yako kufanya kitu ambacho hukipendi, tafuta Biashara ambayo unayopenda kuifanya ili uwenza Leo kuifanya Biashara hiyo. Siri kubwa ya Mafanikio kwenye Maisha ni kufanya Biashara ambayo unaipenda Kwa sababu inakupa nguvu na Hamasa ya kuifanya bila kuchoka. Kwhyo kuanzia Leo kaa Chini ujiulize ni Biashara gani ambayo ninaipenda kuifanya , baada ya Kupata jibu ndio jipangie siku ya kuanza kuifanya Biashara yako . Jitahidi usichelewe kuanza Biashara yako kwani Ukichelewa kuanzisha Biashara yako ndio unachelewa kufanikiwa .
Anza Leo ili Ufanikiwe Leo.

2.Fanya kazi Kwa bidii:

* Katika Biashara bidii inahitajika sana ili kufanikiwa Katika Maisha yako. Unatakiwa kujitowa, kujituma
Usijionee huruma wakati unatafuta Mafakio, jionee huruma kawann sijapata Mafaniko.
Wakati wa kutafuta Mafakio unatakiwa Ujitowe na wala usijionee Huduma , saivi hangaika kutafuta Mafakio yako na baada ya Kupata Mafakio ndio utakuja kupumzika na kutulia
Anza Leo kufanya Kazi Kwa bidii ili UJIPATIE Mafanikio ya Haraka 


3.Fanya kazi Kwa ubora

:* Hii ni Mbinu kubwa sana yàa mafanikio, ubora ndio unaokufanya ujipatia Mafakio Kwa muda mfupi.
Haijalishi unafanya kazi gani, popote ubora unahitajika.
Kama unafanya Biashara ya Juice jitahidi Juice yako iwe tamu na mzuri, kama unauza Vyakula jitahidi Vyakula vyako viwe vuizuri na vitamu, kama unauza Nguo Jitahidi Nguo zako ziwe mzuri na zenye kupendezesha, Biashara yoyote unayoifanya ubora unahitajika.

4.Tangaza Biashara yako:

kama hutangazi Biashara yako hakuna Mtu ambae atajua kuwa wewe unafanya biashara gani, ndio maana unaona hujipatii Wateja kwenye Biashara yako na kusema hakuna Wateja kumbe sio kweli, kumbuka Wateja ni wengi sana na huwezi kuamaliza 
Tumia Mitandao ya kijamii kutangaza Biashara yako, kama Instagram, Facebook, Whasap n.k, kupitia Mitandao ya kijamii  Kwa kutangaza Biashara yako utajipatia Wateja wengi sana Kwa muda mfupi Tu. 
Pia wambie Marafiki zako kua wewe unafanya Biashara gani ili wawe wateja wako na waweze kukutafutia wateja wengine zaidi. 


5.Kua na nidhamu ya Pesa

zingatia sana kanunui hiiPesa huwezi kushindana nao lazima itakushinda tu .Kila siku unatakiwa ujiwekee Akiba ili baadae uwe na Uhuru wa kifedha Katika Maisha yako.
Lazima ukae Chini ujipangilie Kwa siku utaweka Akiba Kiasi gani?, Kwa wiki utaweka Akiba Kiasi gani? , Kwa Mwezi utaweka Akiba Kiasi gani?, Kwa mwaka utaweka Akiba Kiasi gani? . Kama huwez kujiwekea Akiba kumbuka unaelekea kwenye Umasikini.
Jilazimishe kueka Akiba kwenye Maisha yako ili ujipatie Mafaniko Makubwa mbeleni na kua na Uhuru wa kifedha .
Kuweka Akiba sio kitu Rahisi lazima ujilazimishe , Kumbuka ukijilazimisha kitu chochote utaweza kufanya , usikubali kufanya kitu Kwa kujiskia fanya kitu Kwa kujilazimisha ili utilize Malengo yako.

6.Ongeza Kipato chako:

 usikubali kua na Kipato kimoja tu Kwani kua na kipato kimoja ni dalili tosha  ya kua hutaki Mafanikio unataka kua masikini kwenye Maisha yako.
Kumbuka kipato hakiwezi kuongezeka lazima uamue wewe mwenyewe kuongeza kipato chako.
Usiishi Kwa kutamani tu bali chukua hatua ili kutimiza MALENGO yako.
Utaskia watu wengine wakisema, mm sina Mtaji mkubwa wa kuanzisha biashara kwhyo nasubiria Mtaji wangu uwe mkubwa, hiyo ni dalili moja wapo  ya kua masikni kwenye Maisha yako 
Kumbuka kwenye biashara kuna Biashara kubwa na ndogo , tafuta Biashara yoyote ambayo utaweza kuifanya Kwa Mtaji uliyo nao. Hata kama Una Mtaji wa sh *10,000* ukiamu kuanzisha biashara  utafanikiwa
Tafuta Biashara za Mtaji Uliyonao  Kwasasa lazima utazipata , kama huwezi kuifanya wewe hiyo Biashara tafuta Wafanya kazi ambao unawaamini ili wakufanyie Biashara zako than utawalipa baada ya Biashara kumaliza au utawalipa Kwa Mwezi na wewe utajipatia kipato chako kupitia wafanya KAZI wako. Ukiona Biashara yako inakua vizuri jitahidi kuongeza Wafanya KAZI wako ili kupanua Masoko yako na kujiongezea kipato zaidi na zaidi 

*AHSANTE SANA*


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA UPISHI MZURI WA KACHORI ZA VIAZI KWAAJILI YA FAMILIA NA BIASHARA😋

JINSI YA KUPIKA SKONZI LAINI NA TAMU