JINSI YA UPISHI MZURI WA KACHORI ZA VIAZI KWAAJILI YA FAMILIA NA BIASHARA😋

Mapishi ya kachori ni rahisi Sanaa na hayahitaji gharama kubwa sana katika kutayarisha lkn pia hayatumii gharama kubwa hadi kukamilisha upishi huo.....

✨Haya sasa tuanze somo letu:

Vipimo: pamoja na viungo☺ 

✓ Viazi   Mbatata (Mviringo)            Kilo 1     

✓ Kitunguu saumu(thomu) na Tangawizi    Kijiko 1 cha chakula

✓ Chumvi    kijiko 1 cha Chakula                                            

✓ Pilipili ya kusaga     kutegemea na unavyoipenda

✓ Ndimu                     1                             

✓ Mafuta ya kupikia kiasi 

✓ Unga wa dengu au Ngano           Kiasi 


NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

➖Chemsha viazi  mpaka viwive, kisha vitoe maganda na uviweka ndani ya bakuli/ Sinia

➖Vipondeponde kwa mkono mpaka viwe laini.

➖Saga thomu na tangawizi kisha changanya na viazi vyako  ulivovuruga  .

➖Weka chumvi, ndimu na pilipili ya unga kwenye Viazi vyako ambayo tayr umeshavuruga then changanya Kwa pamoja  kisha uonje, unaweza kuongeza viungo hivi kwa kadri ya mapenzi yako.

➖Tengeneza madonge ya duara kachori zako  uyapange katika tray/ sinia . Usifange Madonge Makubwa Sana angalia kwenye picha hapo ili ujionee saizi ya Madonge / kachori 

➖Vuruga unga  wa dengu au ngano kwa maji uwe mwepesi kidogo na kua Rojo weka pembeni.

➖Weka mafuta ya kupikia ndani ya karai na uliweke kwenye moto hadi Mafuta yaanze kupata kiasi ndio Uanze kuchoma kachori zako 

➖Chovya madonge /Kachori zako  kwenye rojo la unga kwanza  halafu  uyatose kwenye mafuta ya moto. (Uchomaji wake ni kama kuchoma bajia) 

➖Wacha kachori  zibadilike rangi kuwa ya njano na uzitoe kwenye mafuta.

➖Ukipenda huu Unga wa Ngano ambao umefanya rojo Kwa ajili ya kuchovya kachori zako kabla ya kuingiza kwenye Mafuta unaweza kuingiza rangi unayopenda ili kachori zako ziwe na rangi , kama nyekundu , njano, n.k

➖Weka Kachori  kwenye sahani zipoe tayari kwa kuliwa.

👇👇

Hii ni Biashara Mzuri Sana , unaweza kuifanya Biashara hii hata nyumbani kwako na Watoto wakanunua, Watoto wanazipenda mno ila kama unataka kufanya Biashara usiweke pili pili nyingi Sana. Pia Kwa nyumbani ni mlo mzuri Kwa Asubuhi ukipata  na chai yako itakua poa sana😋😋



*TAMU* 😋😋🥰

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUPIKA SKONZI LAINI NA TAMU