JINSI YA KUPIKA SKONZI LAINI NA TAMU

jinsi ya kupika skonzi laini na tamu:

 Vipimo:

 ✳️Unga -; 4 Vikombe vya chai 

✳️Sukari -; 4 vijiko vya chakula 

✳️Chumvi - 1 Kijiko cha chakul 

✳️Hamira - 1 Kijiko cha chakula ✳️Siagi - ¼ Kikombe cha chai 

✳️Maziwa -; 1 ½ Vikombe vha chai(siyo lazima unaweza tumia maji pia 

🔹Yai; 1 Moja 

🔹Ufuta Kiasi ya kunyunyizia juu . . 

💟Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 ☑️Katika bakuli changanya vipimo vyote isipikuwa ufuta.

 ☑️Kisha ukande unga huku unanyunyizia unga ukiwa unashika

 ☑️Funika mchanganyiko na weka pahali penye joto hadi iimuke.Halafu fanya viduara na viweke kwenye treya ya kuchomea iliyopakwa siagi. 

 ☑️Ziache mahali penye joto hadi zimuuke kwa mara ya pili.

 ☑️Washa oveni moto wa 350°.Pakiza (brush) Yai uliopiga au maziwa juu ya vile vidonge kisha nyunyizia ufuta juu. 

☑️Kisha vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 hivi au kama unatumia jiko la mkaa palia kama upaliavyo wali chini acha moto; kidogo na juu weka mfuniko wenye makaa ya moto na kaa dakika 20 hivi kisha chungulia kama zimekua za brown na kugeuka rangi zitakuwa tayari kuliwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA UPISHI MZURI WA KACHORI ZA VIAZI KWAAJILI YA FAMILIA NA BIASHARA😋